Jumapili 6 Septemba 2026 - 10:04
Hawzah ya Ayatullah Ka'dhimi Yafunguliwa Mjini Ka'dhimain; Hatua Mpya katika Kukuza Elimu za Hawza

Hawza/ Jiji takatifu la Ka'dhimain Iraq, limeshuhudia hafla ya uzinduzi wa “Hawza ya Ayatullah Sheikh Muhammad Hussein Ka'dhimi” kwa ajili ya masomo ya elimu za Hawza, iliyofanyika jirani na eneo walilozikwa Maimamu wawili, Imam Jawad na Imam Ka'dhim (as).

Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, jiji takatifu la Ka'dhimain, jirani na eneo walilozikwa Maimamu wawili, Imam Jawad na Imam Ka'dhim (amani ya Mola iwe juu yao), limeshuhudia hafla ya uzinduzi wa “Hawzah ya Ayatullah Sheikh Muhammad Hussein Ka'dhimi” kwa ajili ya masomo ya elimu za Hawza. Hafla hiyo imefanyika sambamba na kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Mtukufu Muhammad (rehema na amani za Allah ziwe juu yake na Ahlulbayt zake) na Imam Jaafar Sadiq (as), huku ikihudhuriwa na walezi na wajumbe wawakilishi kutoka katika Ataba Takatifu na maeneo matukufu, pamoja na kundi la wanazuoni wakubwa, walimu wa Hawza na wanafunzi wa elimu ya dini.

Ujenzi wa jengo hili la kielimu umefanyika kwa amri ya Marjii Mkuu wa Iraq, Ayatullah Sayyid Ali Husayni Sistani, ili kuongeza kituo cha kielimu na kimaarifa katika mazingira ya kielimu ya jiji takatifu la Ka'dhimain, na pia kushiriki katika kuimarisha mkondo halisi wa Hawza ya jiji hili, ambayo kwa karne nyingi imekuwa ikibeba jukumu la kulea na kuendeleza elimu za dini, kuwaunga mkono wanafunzi na kueneza maarifa ya Ahlulbayt (amani ya Allah iwe juu yao).

Hawzah ya Ayatullah Ka'dhimi Yafunguliwa Mjini Ka'dhimain; Hatua Mpya katika Kukuza Elimu za Hawza

Katika hafla ya uzinduzi, hotuba kadhaa zilitolewa, zikijadili umuhimu wa kielimu na kihistoria wa mradi huu pamoja na nafasi yake kama mwendelezo halisi wa harakati za kielimu katika jiji takatifu la Ka'dhimain; jiji ambalo katika historia yake yenye utajiri limejulikana kwa kuwavutia wanazuoni, mafaqihi na watafiti, kuwa mwenyeji wa hawza za kielimu, pamoja na kutumia mitaala madhubuti na yenye kina ambayo imesaidia kuimarisha elimu za Aali Muhammad (as) na kulea vizazi vya wanafunzi wa hawza.

Katika hotuba hizo ilisisitizwa kwamba: Uzinduzi wa hawza hii ni kituo kipya katika njia ya kuhudumia elimu na maarifa, na chanzo muhimu katika harakati za Hawza. Aidha, hawza hii ni jengo la kidini na kielimu linaloongezwa katika orodha ya miradi inayochangia kuimarisha nafasi ya jiji takatifu la Ka'dhimain kama ustaarabu mashuhuri wa kielimu na kimawazo, na moja ya vituo vya kung’arisha maarifa na fikra katika ulimwengu wa Kiislamu.

Uzinduzi wa “Hawza ya Ayatullah Sheikh Muhammad Hussein Kazimi” (ra) ni uthibitisho wa kina wa urithi wa kielimu uliotunzwa katika jiji takatifu la Ka'dhimain, pamoja na mwendelezo wa njia ya jiji hili katika kuhudumia elimu za dini na kuimarisha uwepo wake wa kielimu. Hali hii inaendana na nafasi yake ya kihistoria na jukumu lake katika kuandaa wanazuoni wa Hawza pamoja na wanafunzi wa elimu na maarifa kwa ajili ya mazingira ya Kiislamu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha